Tuesday, February 3, 2009

Maisha yangu

maisha yangu yalikuwa ni ya kawaida katika miaka yote niliyoishi hapa Tanzania

DODOMA,
SERIKALI imezitaka zahanati za watu binafsi nchini kuwatibia haraka wagonjwa mahututi wanaofikishwa kwenye vituo hivyo kabla ya kutoa malipo.Mwito huo umetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Bwana Aggrey Mwanri, wakati akijibu maswali ya wabunge katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Naibu Waziri Mwanry, amesema hospitali hizo zinatakiwa kuzingatia zaidi usalama wa wagonjwa na kanuni za afya wakati zinapotoa huduma badala ya kujali faida itokanayo na biashara hiyo.

Amewataka wamiliki na watumishi wa hospitali hizo kuzingatia zaidi kuokoa maisha ya wagonjwa hata kama hawana pesa za kutoa mara wanapofikishwa kwenye vituo hivyo kwa ajili ya matibabu.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mwanry, amesema Serikali bado inaendelea na utaratibu wa kutoa bure huduma za afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka Mitano, wazee wenye umri kuanzia miaka 60 na wanawake wajawazito.

No comments:

Post a Comment